Menu
 

Usain Bolt amedhamiria kuingie kweli kwenye mchezo wa soka ili kutimiza ndoto zake.

Baada ya mwezi January ya mwaka huu Bolt kutua Afrika Kusini na kufanya mazoezi kwenye klabu ya Mamelodi Sundowns, sasa ametua Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Mwanariadha huyo mwenye rekodi za kipekee duniani, ameanza kufanya mazoezi na Dortmund Alhamisi hii akiwa na wachezaji mastaa wa timu hiyo akiwemo Marco Reus, Mario Gotze, André Schürrle na wengine.

Mwezi January wakati akiongea Daily Express, Bolt alisema mwezi March atafanya majaribio na Dortmund na ndiyo itaamua kama ataweza kufanya kazi hiyo ya kucheza soka.


Post a Comment

 
Top