Menu
 

Kisukari ni ugonjwa wa kongosho, wakati uzarishaji wa Insulini au utolewaji wake haufanyi kazi vizuri, na ikiwa hali hii haitadhibitiwa, inaweza kusababisha matatizo makubwa kwenye macho, figo, neva, mishipa ya damu, Ini na moyo.

Insulin ni nini?

Insulin ni homoni inayotoa ishara kwa seli za mwili ili ziweze kuchukua glucose kotoka kwenye damu na kuitumia katika kuupa mwili nguvu na kuujenga. Kama kiwango cha insulin mwilini ni kidogo au hakuna insulin kabisa katika mwili, glucose haitachukuliwa na seli za mwili hivyo kusababisha mwili kuyeyusha mafuta yaliyomo mwilini ili upate nguvu.

Kuna aina kuu mbili za kisukari:
• Kisukari aina ya kwanza, ambapo Insulini inakuwa tegemezi (insulin-dependent); hapa kongosho halitengenezi kabisa insulini au linaitengeneza kwa kiasi kidogo sana kiasi kwamba mgonjwa analazimika kuchomwa sindano ya insulini au kutumia pampu za insulini.

Aina ya kwanza ya kisukari inaweza kutokea kwa watu kuanzia utotoni mpaka kwa watu wa umri wa miaka 30. Aina hii ya kisukari hushambulia kwa haraka sana, kwa kawaida ndani ya majuma mpaka miezi kadhaa.

Kwakuwa kongosho halifanyi kazi vizuri, usawa wa damu sukari lazima upewe uangalizi wa karibu. Watu wenye kisukari aina hii ya kwanza pia huwa na uzito pungufu (underweight).

• Kisukari aina ya pili ni wakati ambapo insulini inakuwa huru (insulin-independent) au inapatikana lakini kongosho haliitoi na hivyo dawa (kemikali) lazima itumike kulilazimisha kongosho kutoa insulini.

Aina ya pili ya kisukari huanza kujitokeza kuanzia umri wa miaka 40 na kinachosababisha ni miaka mingi ya kula chakula kisicho sahihi, kutofanya mazoezi au sababu za kurithi (genetics). Watu wenye kisukari cha aina hii ya pili pia huwa na uzito uliozidi (overweight).

Chanzo: Fadhil Paulo na mtandaoni

Post a Comment

 
Top