Menu
 


Manchester United wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk Fred, 25, na wana matumaini ya kukamilisha shughuli hiyo ifikapo wiki ijayo. (Manchester Evening News).

United wameanza mazungumzo na Tottenham ya kumsaini mlinzi Toby Alderweireld, 29, lakini Tottenham wanataka pauni milioni 75 kwa mbelgiji huyo. (Mirror).

 Mchezaji anayewindwa na Manchester City Jorginho, 26, atafanya mazungumzo na Napoli wiki ijayo huku Mbrazil huyo anayewekewa thamani ya pauni milioni 52 akiwa na nia ya kuhamia klabu ya Premier League. (Sun).

 Manchester City watahitaji kulipa pauni milioni 60 kumsaini winga wa Leicester Riyad Mahrez, 27, ambaye walijaribu kumsaini mwezi Januarai. (Guardian).

Atletico Madrid na Inter Milan wote wanataka kumsaini mshambuliaji wa West Brom Salomon Rondon, 28, na raia huyo wa Venezuela anapatikana kwa pauni milioni 16 baada ya klabu hiyi kuondolewa kutoka Premier League. (Sky Sports).

Atletico wamempa ofa mshambuliaji wao wa umri wa miaka 27 Antoine Griezmann pauni milioni 8.75 zaidi ya Barcelona ili Mfaransa huyo apate kubaki katika klabu hiyo. (Mail).

Post a Comment

 
Top