Menu
 Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 26, amesema wazi wazi anatataka kuondoka Real Madrid msimu huu wa joto , mwaka mmoja baada ya Mbrazil huyo kujiunga na mabingwa hao wa Ufaransa. (Goal)

Chelsea wamemuorodhesha mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 29, miongoni mwa wanaowataka kuwasajili msimu huu. (Telegraph)

Manchester United wanamatamanio ya kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Willian, 29, msimu huu wa uhamisho. (Sky Sports)

Lakini Manchester United wako tayari kujiondoa kwa uhamisho wa £53m wa Shakhtar Donetsk na kiungo wa kati wa Brazil Fred ,25. (Metro)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Manchester United Anthony Martial, 22, ananyemelewa na mahasimu wao wa ligi ya Premia Tottenham. (London Evening Standard)

Barcelona wanapanga kusamjili mshambuliaji wa Spurs Reo Griffiths katika uhamisho wa msimu huu wa joto. (Star)

 AC Milan wana mpango wa kumsaini mshambuliaji wa Chelsea rai wa Uhispania Alvaro Morata, 25. (Sky Italia - in Italian) 

 Unai Emery hatakuwa na ushawishi katika kuwanunua na kuwauza wachezaji wakati atateuliwa meneja wa Arsenal. (Mirror)

 Emery ana nia ya kumweka kiungo wa kati Aaron Ramsey, 27, katika mipango yake licha mchezaji huyo kuhusishwa na mpango wa kukihama klabu hiyo. (Sky Sports)

 Manchester United wana nia ya kusikiliza ofa kwa mshambuliaji raia wa Ufaransa Anthony Martial, 22, lakini wako makini wasije wakamuuza kwenda klabu pinzani ya England. (Mail)

Post a Comment

 
Top