Menu
 

Usiku wa jana umefanyika ugawaji wa tuzo za soka katika ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1.

Katika tuzo hizo Paris Saint-Germain imefanikiwa kunyakuwa tuzo kubwa zote ikiwemo ya mchezaji Bora wa ligi hiyo iliyokwenda kwa Neymar Jr.

Neymar ameshinda tuzo hiyo akiwa amecheza mechi 20 msimu huu na kufunga mabao 19 pamoja na kutoa pasi za mwisho 13.


Wakati huo huo Kyllian Mbappe ametwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa mara ya pili huku akiwa mchezaji wa pili kufanya hivyo kwenye historia ya ligi ya Ufaransa baada ya Eden Hazard.

Naye kocha wa timu ya PSG ambaye anamaliza muda wake, Unai Emery ameshinda tuzo kocha bora.

Post a Comment

 
Top