Menu
 

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kusema hana bifu lolote na staa wa muziki wa Bongo fleva Harmonize hata baada ya kumdhalilisha mume wake.

Wiki chache zilizopita Harmonize alikuwa kwenye vita kali ya Ex wake Jacqueline Wolper na katika ugomvi wao alimtaja mume wa Shamsa Chidi Mapenzi kama mmoja wa mpenzi wa zamani wa staa jambo ambalo lilimkera Shamsa.

Shamsa aliweka wazi kuwa hajafurahishwa na maneno ya Harmonize kumuingiza mume wake Kwenye bifu lake na Wolper na kumdhalilisha wakati anajua wazi kuwa ameoa tayari.

Kwenye mahojiano na FNL ya EATV, Shamsa amesema kuwa licha kutopendezwa na kitendo hicho kwa ujumla hana ugomvi na Harmonize ili maisha mengine yaendelee.
"Mume wangu ni mtu mpole sana, inawezekana hakupendezwa ila alikaa kimya, sisi wanawake tunamunkari ya hali ya juu, halafu unaona huyo kapata wapi huo ujasiri wa kuweka hivyo bila kufikiria hawa watu wengine tayari wana familia zao.

Nilipaniki lakini mwisho wa siku simchukii na sina bifu naye niliongea nilichokuwa najisikia na yameisha na hata tukikutana tunasalimiana vizuri kwa sababu hatuna bifu. Sisi ni vijana tunahitaji kuweka nguvu nyingi sana katika kufanya kazi na sio mabifu”.

Post a Comment

 
Top