Menu
 

Matajiri wa Ufaransa klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) imethibitisha kumteuwa, Thomas Tuchel kuwa kocha mpya wa timu hiyo.

Mjerumani huyo alikuwa nje ya uwanja tangu aondoke ndani ya klabu ya Borussia Dortmund msimu uliopita wa majira ya joto.

Taarifa kamili kutoka ndani ya klabu hiyo kupitia mtandao wake wa Twitter umethibitisha , Tuchel kusaini mkataba wa miaka miwili ndani ya PSG na kuchukua mikoba ya Unai Emery.

Post a Comment

 
Top